Zuwena

Diamond Platnumz

Mnh!
Habari gani kaka naamini unanisikia
Mi mzima wa afya mama mungu anasaidiaToka ulipotuacha mahututi anazidiwa
Bibi presha presha nae akatangulia
Bado twakuombea ulale salama pema
Japo moyoni nna dukuduku
Natamani kusema, niseme eeh
Zile mali wosia ulizotuhusia Tuligawa salama
Zuwena zote tukampatia Tusiwe ndugu lawama
Ila... Zuwena kaka, amebadilika sana
Yani shem lake bi Zuuh wa leo
Sio yule wa jana

Natamani ungemuona (Zuwena)
Japo ungemuona (Zuwena)
Kidogo tu ungemuona (Zuwena)
Ungemuoona (Zuwena)
Ooooh ungemuona (Zuwena)
Ahh zuwena (Zuwena)
Ooooh ungemuonaa (Zuwena)
Zuwena oooooh

Mmh Zuwena sasa kawa chotara
Sio tena cheusi mangara
Ngozi kaichubua awe Muzungu
Anavuta na sigara
Mara Boko, Mwananyamala
Anachezesha tu miamala
Kutwa anaisugua kipepe rungu
Tena peku bila ndala
Zuwena skuizi anabandika kope (Zuwena)
Zuwena mipasuo kama yote (Zuwena)
Oooh Zuwena, lipa shika tuondoke (Zuwena)
Ahh Zuwena wanamuita chawote ooh ooh
Juzi kabebwa kwa jirani ata hajitambui (Zuwena)
Yani kalewa tafarani kautwika mbwii (Zuwena)
Zuwena sio tena wa ibada na dini
Sadaka chenji asaidie
Skuizi kageuka pedeshee wa mjini
Kutunza bendi wamsifie
Na lile gari lako urithi wa babu
La kulishia ng′ombe
Skuizi kama kwato kwenye vilabu
Linabebea pombe
Mama tete kitandani hawezi ata kutembea
Zuwena ameshindwa ata kuja kumuona
Panadol kumletea

Natamani ungemuona (Zuwena)
Japo ungemuona (Zuwena)
Kidogo tu ungemuona (Zuwena)
Ungemuoona (Zuwena)
Ooooh ungemuona (Zuwena)
Ahh zuwena (Zuwena)
Ooooh ungemuona (Zuwena)
Zuwena oooooh

Skuizi kataradadi anadanga
Anakula ndizi kwa maganda
Anajiita J Lo, Anadanga
Anakula ndizi kwa maganda
Eti Mzungu mweusi anadanga
Anakula ndizi kwa maganda
Na anatunyoosha Baba anadanga
Anakula ndizi kwa maganda