Utanipenda

Diamond Platnumz

Tanta lala la
Ooh la la la la la
Mmh
Ooh Ghafla visenti sina nimerudi Tandale
Nimeshindwa kulipa bima nimeuza Madale
Radio nyimbo wamezima Tv ndio hataree
Umeneja umebaki jina
Hanitaki hata Tale

Oooh wale shabiki zangu
Walionisifu kwa maneno matamu
Leo maadui zangu
Ni mitusi tu kwa instagram

Kimwanaa si dada angu
Eti nae hanifahamu
Hata Harmonize nikimpigia
Ananifokea kama Sallam

Na magazeti ya nyumbani kwa kukuza habari si unajuagaa
Utasikia Tafalani eti Mondi kwa Zari amemwagwa
Navyo nilivyo mnyonge tabia ya kuwajibu sinagaa
Kama naiona michambo ya madem wa zamani nlio wapitiaga

Ooh nayosema yana maana
Sababu hakuna anaejua kesho
Anaepanga ni Rabana
Ila ameificha ni confidential
Ukisali omba sanaa
Mumeo nisije kuwa kichekesho
Maana rafiki wa jana
Aaah
Ndio adui mkubwa wa kesho

La la la la la la
Au je utanipenda gaa?
Aa La la la la la
Au nawe utanimwagaa?
Aa La la la la la
Ati utanipenda gaa ooh
Aa la la la la la

Oh
Bado naiwaza sana
Vile tunzo mashauzi airport
Je itapofika tamati
Utadiriki hata japo kunipost
Pindi show zimekwamaa
Na nikipata sijahis ni mikosi
Oooh jahazi limezama
Mola ninusulu baba

Kama namuona mwanangu
Roho yangu
Tiffa Dangote
Anakwenda na mamaangu
Kwa Jakaya Kikwete wanafukuzwa watoke

Usilie Sandra wangu
Mboni yangu
Jikaze usichoke
Huenda kesho zamu yangu
Nitavuma tena mambo yanyooke

Ey
Na magazeti ya nyumbani
Kwa kukuza habari si unajuagaa
Utasikia tafalani eti Mondi kwa Zari amemwaga (Oh yeh yeh yeh)
Navyo nilivyo mnyonge
Tabia ya kuwajibu sinaga
Kama naiona michambo ya madem wa zamani
Yani He he he

La la la la la (eh)
(Ola lala la lala)
La la la la la
(Ooh ola la la la)
La la la la la ala
Eeeh
Ola la la lilaa ooh

I say
Kama namuona mwanangu
Roho yangu
Tiffa dangote
Ana kwenda na mama angu
Kwa mkubwa Fella anafukuzwa watoke

Usilie sandra wangu
Mboni yangu
Jikaze usichoke
Huenda kesho zamu yangu
Nitavuma tena
Mambo yanyooke(he he heee)

Nayosema yana maana
Sababu hakuna anaejua kesho
Anaepanga ni Rabana
Ila ameificha ni confidential
Ukisali omba sana
Mumeo nisije kuwa kichekesho
Maana rafiki wa jana
Ndio adui mkubwa wa kesho