Mi na wewe
Tuko pamoja
Kama vile tuna swerve
Sema nami mwenzio (mwenzio)
Ukimya sio rafiki wanimaliza moyo
Sema nami kwa vituo
Ukishusha, pandisha pumzi
Mate yateremke taratibu kwenye koo
Sema nami kwa upole
Kama anavyosemezwa mtoto (kama mtoto)
Usininyooshee kidole
Nishike, nibembeleze kidogo
Sema nami ukicheka
Macho yakitabasamu (tabasamu)
Kama kiziwanda nikideka
Ndivyo maongezi yawa matamu
Sema nami nijaze hamu
Ya kubonga nawe kila siku
Wengine waombe zamu
Iwakamate shauku
Kuna zam, zam, zam, zam
And I just want, mambo matam
Mi na wee kama vile tuna swervin away
Mi na wewe kama vile tryna getting our way
It′s like, both you and I
Both you and I, eh
Skia, eh
Wait, eh
Stop, eh
Let me, eh
Take your hands like this and
Both you and I, I
Sema nami kwa ile sauti
Ile, inayonipa njozi
Wakinikuta mahututi
Ujue sababu ni hayo mapozi
Sema nami uwe mkombozi
Wa huzuni na majonzi yangu
Sema nami jaka moyo
Lisikumbatie nafsi yangu
Sema nami kwa vituko
Nicheke nipate afya
Mwili uingiwe muamko
Nikohoe, nikipige chafya
Sema, we sio kibogoyo
Maneno waweza unda
Usiwe na choyo
Sikio lataka lake tunda
Sema nami kwa hisia
Nizame kama majini
Sema nije hadithia
Uniwekavyo makini
I like it when you're playful like a teenage boy
I like it when you get a little coy
When you set a little ploy
Make me chase you up for a convo
Wewe ndiyo chanzo
I sleep late night
Just to hear you feels right
We ain′t never gonna' fight like this
Ukinipa maneno yako tight like this
Baby, just like this
Sema nami
Twende sawa kwa hatua
Go slow, don't rush
Meza mate, pumua
And give my hungry ears a little tour (hungry ears a little tour)
Sema nami
We sema, sema nami
Oya, sema na mimi basi
Hivi, unaniskia kweli?
Tusemane a′fu mi nikisema freshi tu
Sema nami basi, come on!