Mapenzi

Kidum

Uh uh uuh uuh, eeh

Mapenzi yo yo yoKama ni mapenzi
Ya kuniudhi kila saa
Ya kunifanya mi kulia
Na kama huridhiki
Na mbona hujasema
Ili niweze rekebisha
Nilidhani mambo shwari
Nikiamini u kwangu
Na kukusifu kwa wazazi
Hujali tena hisia zangu

Sijui tunapokwenda
Lakini najua tulipotoka
Kutoka sitoki nimetekwa nyara
Kukuwacha siwezi kibarua ngumu
Nashindwa ni nini nitafanya uridhike
Nimetekwa ndani

Mtandao wa mapenzi

Basi nakuomba
Uniteke tu bila mateso
Nimezama, nimezama
Ndani ya bahari, la penzi lako
Siwezi, kusonga mbele
Kurudi nyuma, sielewi
Haya mapenzi ya fujo hayafai
Kama unanipenda
Jaribu kunipa raha

Mi nashangaa
Watu wakisema
Eti tunapendana
Japo tunazozana
Ni vizuri mamii
Nyumba kuwa na siri
Lakini jaribu, tusuluhishe
Bila hivyo
Itakuwa mchezo, wa kuigiza

Kwenye mambo bandia
Mimi sitaki
Mambo ya kujifanya
Eti tunapendana
Tena tunatesana, uuuh
Nimejaribu sana kujitoa ndani (aah aah)

Kila nikipanga napangua mwenyewe (aah aah)
Natamani sana ungeelewa hivyo
Mimi mateka
Mimi pumbavu
Wa penzi lako
Nieleze ni lini ntakuwa huru

Tazama, nimezama (tazama yooh)
Ndani ya bahari, la penzi lako
Siwezi, kusonga mbele
Kurudi nyuma, sielewi
Haya mapenzi ya fujo hayafai
Kama unanipenda
Jaribu kunipa raha

Jaribu baby, uuh woo
Mambo, ya kunifanya kumbafu haifai
Mambo yo yo yo yo yo yo yo

Haifai
Jaribu baby
Tusuluhishe

Daftar lirik lagu Kidum