Mwenyewe

Harmonize

Cough
Yao yaoo
Mmmh mmmh mmmhAlrighty

Tisini na nne march fifteen
Beginning of my world
Nilipozaliwa nikadondoka chini
Hakukua na kitanda kwa ward

Basi mgongo wa mama nikaufanya godoro
Na kilichonikuza mihogo na viporo
Nilipelekwa shule ila bado nikawa mtoro
Kingereza nilichokalili labda tomorrow ama today

Zikafika time ya kubalehe
Nikayajua mapenzi nikagundua bila pesa siyawezi
Ni ujinga

Nikadondokea umachinga
Hapakuchi panakucha siku zikasogea
Pruuh mpka dar es salaama nikaanza jitegemea
Nyumbani baba na mama wakiniombea

Mwanetu nenda salama na ukipata rejea
Mmh na ukipata
Hapo akili ndo ikaanza kukomaa
Na nikajuta kwanini sikusomaa

Jinsi jua la utosi linavyochoma
Na usiku baridi ikanipa homa nusu inuchukue uhai mmmh
Mi nimepitia mengi ndo mana sio mshamba wa helaa
Kwa ajili ya vitu vidogo sigombani na maselaa

We kubali kudharauliwa
Kukataliwa
Kupata majaliwa
Kula kinacholiwa(mwenyewe)

Raha jipe mwenyewe
Basi kamata chupa fungua na mimina(mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe
Lewa tukuone unavyocheza kichina(mwenyewe)

Raha jipe mwenyewe
Anaekupenda zaidi ni wewe(mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe
Ata anaekujua zaidi ni wewe(mwenyewe)

Raha jipe mwenyewe
Masikini na wanawe tajiri na mali zake
Asie na shida nawe mwache aende zake
Usibweteke na ulicho nacho

Pia usiteseke kwa walicho nacho
Riziki mafungu saba pengine leo zamu ya sita
Kaza moyo epusha roho yakusita
We umezaliwa peke yako

Utakufa peke yako
Na utazikwa peke yako
So usiwaeleze shida zako
Ukidhani ndugu zako kumbe ndo wabaya wako
Wee komaaa(mwenyewe)

Raha jipe mwenyewe
Basi kamata chupa fungua na mimina(mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe
Lewa tukuone unavyocheza kichina(mwenyewe)

Raha jipe mwenyewe
Anaekupenda zaidi ni wewe(mwenyewe)
Raha jipe mwenyewe
Ata anaekujua zaidi ni wewe(mwenyewe)

Raha jipe mwenyewe
Cough
Alrighty
Yaoo yaoo

Daftar lirik lagu Harmonize