Kaa nami ni usiku sana
Usiniache gizani Bwana
Msaada wako haukomi
Nili peke yangu, kaa nami
Siku zetu hazikawi kwisha
Sioni la kunifurahisha
Hakuna ambacho hakikomi
Usiye na mwisho, kaa nami
Nina haja nawe kila saa
Sina mwingine wa kunifaa
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe Bwana kaa nami
Sichi neno uwapo karibu
Nipatalo lolote si taabu
Kifo na kaburi haviumi
Nitashinda kwako kaa nami
Nilalapo nikuone wewe
Gizani mwote nimulikie
Nuru za mbinguni hazikomi
Siku zangu zote kaa nami